Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua kampeni ya kulinda urithi nchini Libya

UNESCO yazindua kampeni ya kulinda urithi nchini Libya

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuheshimu utofauti wa tamaduni katika mazungumzo na maendeleo, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limezindua kampeni ya #Unite4Heritage, inayolenga kuwaleta watu pamoja ili kulinda urithi wao.

Kupitia kwa kampeni hiyo, ambayo ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kuendeleza umuhimu wa urithi wa kitamaduni kama chombo muhimu kwa mazungumzo na amani, UNESCO inawahimiza raia wote wa Libya, hususan vijana, kuanza kufanya mazungumzo kuhusu jinsi wanavyoona mchango na thamani ya urithi wa kitamaduni wa Libya katika maisha yao na katika jamii zao, na kuufahamisha ulimwengu kuuhusu.

Ufahamisho huu unaweza kufanyika kupitia kuweka picha na video kwenye mitandao ya kijamii, kuandaa hafla mbali mbali, au chochote ambacho kinaweza kufanywa ili kupigia debe ukwasi wa urithi wa utamaduni wa Libya.