Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amelaani vikali shambulio la kigaidi kwenye basi mjini Karachi Pakistan

Ban amelaani vikali shambulio la kigaidi kwenye basi mjini Karachi Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea leo kwenye basi mjini Karachi nchini Pakistan na kuarifiwa kukatili maisha ya watu 45 kutoka jamii ya Ismaili na kujeruhi wengine wengi.

Ban ameitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua zozote za muhimu kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na tukio hilo la kikatili.

Kwa kuzingatia kwamba matukio kadhaa ya mashambulizi dhidi ya wakristo na washia wachache katika siku za karibuni , Katibu mkuu ameitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua madhubuti zenye lengo la kuwalinda waumini wa dini walio wachache  nchini humo.

Akiongeza kuwa ni lazima kuwe na mazingira ya kuvumiliana kuelewana na kuheshimiana kwani kutasaidia sana kufikia malengo ya amani.