Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ziweke mipango ya udhibiti wa silaha:Ban

Nchi ziweke mipango ya udhibiti wa silaha:Ban

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala kuhusu madhara ya matumizi mabaya ya silaha ndogo ndogo kwa binadamu ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema udhibiti mbovu wa silaha hizo ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa wakati huu ambapo mizozo inaibuka kila uchao. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ban katika hotuba yake amesema mjadala huo ni muhimu kwani muongo uliopita pekee umeshuhudia mizozo zaidi ya 250 na matumizi ya silaha ndogo ndogo yakishamiri, wanawake, watoto na wanaume zaidi ya Elfu hamsini wakiuawa kila mwaka kutokana na matumizi ya silaha hizo akitaja chanzo..

“Udhibiti mbovu wa silaha unatia wasiwasi. Nchi  nyingi hazina mipango na ufuatiliaji makini ya kuhifadhi, kushughulikia, kusafirisha na kuziteketeza.”

Hivyo akasema kutiwa saini kwa mkataba wa kudhibiti biashara ya silaha duniani, ATT ni mwanzo mzuri hivyo..

“Mosi tuhakikishe vikosi vya taifa vinapotumia silaha vinazingatia misingi na mikataba ya kimataifa, ikiwemo uhifadhi wake. Pili tunahitaji hatua zaidi kudhibiti ueneaji wa silaha haramu.”

Mwingine aliyehutubia ni Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ambaye amesema mara nyingi wahanga wa matumizi wa silaha hizo ni raia wasio na hatia huku wahusika wakikwepa sheria hivyo..

(Sauti ya Zeid)

“Ni lazima tuweke ulinzi wa uhai wa binadamu na haki za binadamu kama kitovu cha mjadala huu.”