Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maeonesho ya Milan kupigia chepuo utokomezwaji wa njaa

Maeonesho ya Milan kupigia chepuo utokomezwaji wa njaa

Suala la kufikia malengo ya kizazi kisicho na njaa ni moja ya yale yatakayoghubika maenesho ya kimataifa mjini Milan nchini Italia ambayo yameanza tangu Mai mosi mwaka  huu na yanatarajiwa kukamilika mnamo Oktoba 31 .

Hii ni kwa mujibu wa kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa meoesho hayo aliye pia msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Eduardo Rojas ambaye ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa kuwa onesho hilo ambalo litashirikisha nchi 130 kote duniani linalenga kuidhihirishia dunia kuwa kumaliza njaa inawezekana.

Akizungumzia zaidi maonesho hayo yenye kauli mbiu lisha sayari, nishati kwa maisha Bwana Rojas anasema

(SAUTI)

"Kwa upande mwingine tuna mada kama washiriki wengine kuhusu kupunguza njaa kama ilivyozinduliwa na Katibu Mkuu mjini Rio de Janeiro."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatarajiwa kuhudhuria maonesho hayo.