Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waadhimisha kengele ya amani

Umoja wa Mataifa waadhimisha kengele ya amani

Hawa ni watoto wanaoimba wimbo “Imagine” wa John Lennon ambao unamaanisha matumaini ya amani kwa dunia, wakati wa hafla maalum iliyofanyika jumatano hii kwa ajili ya kuhamisha rasmi kengele ya amani ya Umoja wa Mataifa.

Kengele hiyo ya amani imerudishwa rasmi kwenye sehemu yake ya awali baada ya kuhamishiwa kwenye bustani ya maua wakati wa ukarabati wa majengo ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, ambao umekamilishwa hivi karibuni.

Katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kwamba kengele hiyo inatuma ujumbe wa amani kwa nchi zote za dunia.

“ Miaka 61 baada ya zawadi ya kengele ya amani, kengele hiyo bado inawakilisha hamu ya wote kwa dunia inayoishi na amani. Tukisherekea leo, tutafakari maneno ya mbunifu wake na tukariri utashi wetu wa kushirikiana kwa ajili ya amani.”

Kengele ya amani ni zawadi ya Shirika lisilo la kiserikali la Umoja wa Mataifa Japan iliyotolewa mwaka 1954 kabla Japan haijakubaliwa kuwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1954. Kengele Inapigwa rasmi kila Septemba, tarehe 21, ikiwa ni siku ya kimataifa ya amani.