Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia-Pacifik kuingia katika mkakati wa ufadhili kwa maendeleo:ESCAP

Asia-Pacifik kuingia katika mkakati wa ufadhili kwa maendeleo:ESCAP

Watunga sera kutoka Asia-Pacific pamoja na wafanyabiashara na wawakilishi wa jumuiya za kijamii kutoka mataifa 40 ya eneo hilo Alhamisi wameafikiana mkakati wa kihistorioa wa ufadhili wa fedha ili kuunganisha rasilimali za kikanda kwa ajili ya ukuaji unaojumuisha wote na endelevu.

Mpango huo wa kikanda ulioidhinishwa katika majadiliano ya ngazi ya juu ya tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na masuala ya kijamii kwa mataifa ya Asia na Pacific ESCAP na serikali ya Indonesia , unaainisha njia mpya za kukusanya rasilimali za kifedha kwa ajili ya kubadili mtazamo wa maendeleo ya kikanda .

Mkakati huo ambao umejikita Zaidi katika nchi ambazo ni miongoni mwa masikini kabisa duniani na zilizo na changamoto za kijiografia , una lengo la kuunda nafasi nyingi za ajira, na kuondoa pengo kubwa lililopo katika nyanja ya kiuchumi na kijamii , kutokuwepo usawa wa kijinsia, tofauti kubwa ya mijini na vijijini, na kuziweka nchi hizo katika msitari wa utekelezaji wa mabadiliko ya ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015.