Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira ya kazi uliko yako salama?

Mazingira ya kazi uliko yako salama?

Wakati siku ya kimataifa ya usalama na afya makazini ikiadhimishwa wiki hii  , Shirika la Kazi Duniani(ILO) limetoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zifanye kazi kwa bidii kuimarisha usalama na afya katika maeneo ya kazi.

Tamko la ILO kwa nchi wanachama linamnukuu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Guy Ryder akisema kuwa sababu za kiuchumi au msukumo wa kupata faida hauwezi kuachiwa uruhusu kupindisha taratibu za kazi na hivyo kuathiri maisha ya mamilioni ya wafanyakazi duniani kupitia vifo, majeruhi au magonjwa kazini.

Takwimu za ILO zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni mbili hufariki dunia kila mwaka katika sehemu za kazi kutokana madhara mbalimbali  huku wengine zaidi ya milioni 300 wakikabiliwa na majeraha . Takwimu hizo zinaonyesha kuwa zaidi ya wafanyakazi 800,000 hujeruhiwa kila siku wakiwa katika maeneo mbalimbali ya kazi

Shirika hilo la kazi duniani limesema kila mtu ana wajibu wa kuzuia  vifo,  majeraha na magonjwa yanayotokea sehemu za kazi na hivyo kuboresha usalama na afya za sehemu za kazi.

Wakati siku hii ikiadhimishwa kimataifa,  mataifa ya Afrika Mashariki mathalani Uganda mnamo Mei Mosi imeadhimisha sikukuu ya wafanyakazi ambayo hutumiwa kuangazia haki na wajibu wa wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi.  Je hali ya usalama katika maeneo ya kazi ikoje nchini  humo? Tuungane na John  Kibego.