UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari Balanga huko DRC

30 Aprili 2015

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO , leo ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kufuatia mauaji ya mwandishi wa habari Soleil Balanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Flora Nducha na taarifa kamili.

 (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa UNESCO mauaji hayo yaliyotokea Aprili 16 mwaka huuu. Bi Irina Bokova Mkurugenzi mkuu wa UNESCO, amesema ameshtushwa saana na mauaji hayo ya kikatili ya  Soleil Balanga, na ameitaka serikali kuhakikisha waliohusika wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ameongeza kuwa vurugu na ghasia haziruhusiwi kuwanyamazisha waandishi wa habari na kuunyima umma taarifa unaozostahili kupata. Balanga aliuawa mjini Monkoto, kwenye jimbo la kaskazini Equateur.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter