Skip to main content

Elimu kuhusu haki za mtoto bado mashaka kwa nchi zilizoendelea:UNICEF

Elimu kuhusu haki za mtoto bado mashaka kwa nchi zilizoendelea:UNICEF

Utoaji wa elimu kuhusu haki za mtoto kwa mujibu wa mkataba wa haki za mtoto duniani, CRC bado ni mashaka katika nchi nyingi zilizoendelea ulimwenguni. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti mpya uliofanyika katika nchi 26 zenye viwanda zaidi duniani kwa ushirikiano kati ya shirika la kuhudumia watoto UNICEF na chuo kikuu kimoja huko Ireland.

Mathalani utafiti huo umeonyesha kuwa ni nchi 11 tu kati ya 26 zinafundisha watoto haki zao kupitia mfumo rasmi shuleni lakini mtaala husika hauna uhusiano na mkataba wa haki za mtoto ikitolea mfano Australia.

Kwa upande wa uwezo wa walimu kutoa elimu  hiyo, ilibainika ni nchi moja tu ambayo inataka mwalimu awe amejifunza vyema mkataba huo ndio aweze kutoa elimu hiyo ya haki za mtoto hivyo ripoti inapendekeza pamoja na mambo mengine.

Dkt. Lee Jerome ni mmoja wa walioshiriki utafiti huo kutoka Chuo Kikuu cha Queens huko Ireland.

(Sauti ya Dkt. Lee)

Mitaala michache sana ina maelezo ya kina ya kile watoto wanapaswa kufahamu na kujifunza kuhusu  haki zao zaidi ya kusubiri walimu wajitokeze na kuwafundisha bila mpango walimu. Halikadhalika hakuna miongozo ya kitaifa ya mafunzo ya ualimu inayohakikisha  uelewa wa walimu wote kuhusu haki za mtoto.”

Mkataba wa haki za mtoto duniani ulianza kutumika mwaka 1990, ukitaja haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa ambapo hadi sasa nchi 191 zimeridhia isipokuwa  Marekani na Sudan Kusini.