Uchafuzi wa hali ya hewa wagharimu dola Trilioni 1.6 kila mwaka Ulaya

28 Aprili 2015

Shirika la afya duniani, WHO kanda ya Ulaya na lile la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, OECD wametoa ripoti yake likisema kuwa uchafuzi wa hali ya hewa barani Ulaya hugharimu dola Trilioni 1.6 kila mwaka kutokana na vifo na magonjwa.

Utafiti huo ulitolewa Jumanne wakati zaidi ya wawakilishi 200 wa Ulaya na mashirika ya kimataifa wakikutana Israel kuangalia mustakhbali wa chombo hicho utatumiwa kudhihirisha athari za mabadiliko ya tabianchi kiuchumi.

Mathalani ripoti inasema gharama ya kiuchumi kutokana na vifo ni zaidi ya dola Trilioni 1.4.

Halikadhalika utafiti huo umebainisha kuwa katika nchi zisizozidi 10 kati ya 53 za ukanda huo, gharama itokanayo na uchafuzi wa hali ya hewa ni asilimia 20 au zaidi ya pato la ndani la taifa.

Kufuatia ripoti hiyo, Katibu Mtendaji wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Ulaya, ECE, Friis Bach akatumia fursa hiyo kusema kuwa kupunguza uchafuzi wa hewa ni kipaumbele cha kisiasa barani humo

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter