Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa UNHCR kuwasili Kathmandu kwa ndege leo:

Msaada wa UNHCR kuwasili Kathmandu kwa ndege leo:

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Shughuli za Dharura, CERF, umetoa dola Milioni 15 kuwezesha shughuli za uokozi nchini Nepal kufuatia tetekemeko kubwa la ardhi lililokumba nchi hiyo mwishoni mwa wiki wakati huu ambapo tayari ndege ya misaada ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR ikiwasili mji mkuu Kathmandu kutoka ghala la shirika hilo lililoko Dubai. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Msaada huu utasaidia huduma ambazo tayari shirika hilo limeanza kuzitoa kwa waathirika wa tetemeko nchini Nepal  katika wilaya mbalimbali.

Watu zaidi ya milioni 8 wameathirika na UNHCR inasema wengi wao wanaishi kambi za muda na maeneo ya wazi kwani nyumba zao zimeharibiwa vibaya au wanaogopa kurejea majumbani kufuatia matetemeko mengine madogomadogo yanayoendelea.

Arianen Rummery ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ARIANE RUMMERY)

“Asubuhi hii wafanyakazi wetu walikabidhi misaada kwa mamlaka za eneo la Sindhuli ambako takribani watu tisa waliuawa na nyumba Elfu tano ziliharibiwa wakati wa janga.  Barabara imezuiwa na maporomoko ya udongo na hivyo tumeweka mpango wa kuhamishia misaada kwenye magari mengine. Timu yetu inaelekea kaskazini-mashariki usawa wa Ramche. Malori manane yanaelekea Okhaldunga kwenye eneo la jirani.”