Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya Posta yabadilike, ubunifu zaidi watakiwa:UPU

Mashirika ya Posta yabadilike, ubunifu zaidi watakiwa:UPU

Mkurugenzi Mkuu wa umoja wa mashirika ya posta duniani, UPU Bishar Hussein amesema sasa ni lazima mashirika ya posta kuangalia upya ni jinsi gani yanatoa huduma zao kwa wateja ili kuweza kukidhi mahitaji yanayoibuka kila uchao.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa kuweka mikakati ya UPU ulioanza Geneva, Uswisi Jumatatu, Bishar amewaeleza washiriki 750 kuwa hatua hiyo ni muhimu na itawezekana tu iwapo wataondokana na mazoea na badala yake kujaribu mbinu mpya bunifu za aina ya huduma na jinsi zinavyotolewa kwa wateja.

Mathalani amesema mabadiliko hayo ni muhimu kutokana na mazingira ambamo huduma zinatolewa akisema sasa huduma za posta  zinajikita zaidi kwenye fedha badala ya barua pekee, halikadhalika mahitaji ya wateja.

Washiriki wanaandaa rasimu ya nyaraka ya mwelekeo wa UPU itakayowasilishwa kwenye mkutano mkuu wa posta huko Uturuki mwaka 2016.