Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala wa sheria na maendeleo endelevu vinaenda sambamba: UNODC

Utawala wa sheria na maendeleo endelevu vinaenda sambamba: UNODC

Amani ya kudumu na maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa iwapo haki za binadamu na utawala wa sheria havitaheshimiwa, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC, Yury Fedotov.

Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wakati wa kongamano la Umoja wa Mataifa la kuzuia uhalifu, linaloendelea mjini Doha, Qatar, Bwana Fedeotov amesema kongamano hilo ni fursa kubwa ya kubadilishana mawazo na kujadili mada hizo muhimu.

“Pamoja tunaweza kuendeleza sheria, kuimarisha utu na kupambana na wahalifu ambao wanakiuka utawala wa sheria na maendeleo endelevu. UNODC iko tayari kushirikiana na mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kufanya bidii ili kutimiza ahadi hiyo”

Bwana Fedetov amezingatia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alioutoa mwanzoni mwa kongamano hilo siku ya jumapili akisema hakuna amani bila maendeleo na wala maendeleo bila amani.