Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yawekeze katika sekta nyingine licha ya ugunduzi wa mafuta na gesi:UNCTAD

Mataifa yawekeze katika sekta nyingine licha ya ugunduzi wa mafuta na gesi:UNCTAD

Ni lazima mataifa hususan yanayoendelea yawekeze katika sekta mbali mbali badala ya mafuta pekee ili kuweza kukabiliana na athari za kushuka kwa bei za mafuta hususan wakati huu ambao kunashuhudiwa kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo duniani. Hiyo ni sehemu ya ushauri aliotoaKatibu Mkuu wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Mukhisa Kituyi alipohojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa kuhusu kongamano la bidhaa za kimataifa linaloendelea Geneva, Uswisi ambapo suala la bei ya mafuta na athari zake katika uchumi limepatiwa kipaumbele. Hapa anaanza kwa kuelezea.athari za kushuka kwa bei ya mafuta.