Tuwezeshe wazee ili wachangie maendeleo ya jamii zao: Ban
Kamisheni ya idadi ya watu na maendeleo imeanza kikao chake cha 48 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York maudhui yakiwa kufikai mustakhbali unaotakiwa kwa kujumuisha masuala ya idadi ya watu kwenye ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kupitia msaidizi wake wa masuala ya uchumi na maendeleo Wu Hongbo akatilia mkazo masuala kadhaa ikiwemo ujumuishi wa wazee kwenye maendeleo akisema.
(Sauti ya Hongbo)
“Idadi ya watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi ikiwa ndio kundi linalokuwa kwa kasi kubwa zaidi, idadi ya wafanyakazi inapungua na watu wanazeeka. Ni lazima tujenge jamii ambazo wazee wanaweza kuchangia zaidi na kufurahia hifadhi ya jamii wanayostahili.”
Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa Babatunde Osotimehin akagusia uhusiano kati ya maendeleo ya vijana na wazee.
(Sauti ya Babatunde)
“Kuwekeza kwenye elimu ya afya na ajira kwa vijana leo ni uwekezaji bora utakaoimarisha maisha ya wazee baadaye.”