Vilabu vya wsikilizaji kwa ajili ya wanawake vyaanzishwa Sudan Kusini

6 Aprili 2015

Katika kukuza uhuru wa kujieleza husuani kwa wanawake Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi, na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na taasisi ya wanawake nchini Sudani Kusini na redio mojawapao nchini humo wameanzisha vilabu vya wasikilizaji wanawake.Vilabu hivyo katika miji ya Rumbek na Wau vinalenga katika kuwawezesha wanawake nchini humo kuzungumza mambo muhimu yanaoyowahusu mathalani elimu kwa msichana na upatikanaji wa maji salama.

Sarah James Ajith ambaye ni mwenyekiti wa taaisis ya wanwake nchini humo amezungumza na Sworo Charles Elisha kuhusu manufaa ya vilabu vya wasikilizaji wa redio

(SAUTI SARAH)

“Klabu ya redio kwa wanawake ni muhimu sana kwa vijana, wasichana na wanawake kwasababu ni jukwaa la kuwaleta wanawake pamoja kwa ajiliya wanawake kuelezea masuala yao pia kuwezesha uwezo wa wanachama wake katika kujiunga na kueleza baadhi ya matatizo yanayowaathiri katika maisha yao.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter