Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN Iraq awatakia wakristo Pasaka njema

Mkuu wa UN Iraq awatakia wakristo Pasaka njema

Sherehe za Pasaka zikiendelea kote duniani, mwakilishi maalum wa Katibu Muu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jan Kubis, amewatakia Pasaka njema jamii ya wakristo waliopo nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, Bwana Kubis amenukuliwa akisema anatumai sikuu hii takatifu inayoadhimisha kufufuka kwa Yesu itafariji mioyo ya jamii ya wakristo ambao, pamoja na watu wengine nchini Iraq, wameteseka kutokana na mwaka mmoja wa mapigano dhidi ya kundi la kigaidi na linalotaka dola ya kiislamu ISIL.

Ameongeza kwamba anatumai mateso hayo yataisha haraka na waliokimbia makwao wataweza kurudi majumbani na kuishi kwa amani na familia, marafiki na jirani zao