Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau duniani elezeeni umuhimu wa michezo kwa maendeleo na amani: UNOSDP

Wadau duniani elezeeni umuhimu wa michezo kwa maendeleo na amani: UNOSDP

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya  maendeleo na amani, shirika la Umoja wa Mataifa la michezo kwa maendeleo na amani UNOSDP limetaka mashirika, wadau na miradi mablimabli inayojihusiha na michezo kueleza namna wanavyotumia dhana hiyo kuleta mabadiliko katika jamii zao.

Kupitia ujumbe wa video, Mjumbe maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa  katika michezo kwa maendeleo na amani Wilfried Lemke ametaka wadua wote kote duniani kuchukua hatua thabiti ya kusambaza  ujumbe wa umuhimu wa michezo akisisitiza

(SAUTI LEMKE)

Michezo imejidhihirisha kama nyenzo muhimu katika ujenzi wa maendeleo na amani.Miradi ya michezo kwa maendeleo na amani duniani imetatua changamoto nyingi duniani ambazo jamii zimekutana nazo. Michezo imekuwa njia muhimu ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia.