Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Singapore yaendelea na maombolezo

Singapore yaendelea na maombolezo

Singapore inaendelea na maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Baba wa Taifa hilo Lee Kuan Yew.

Lee ambaye anajulikana kama Baba wa Taifa la Singapore, alifariki dunia Jumatatu akiwa na umri wa miaka 91.

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Singapore kufuatia kifo cha Lee akimwelezea kuwa amesalia jabali wa bara la Asia na kuwa aliheshimika kwa uongozi wake thabiti.

Halikadhalika amesema alisaidia Singapore kwenye kipindi cha mpito kutoka nchi inayoendelea hadi moja ya nchi zilizoendelea zaidi duniani.

Hayati Lee alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Singapore kwa miongo mitatu hadi alipostaafu mwaka 1990.