Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujangili wa tembo umeendelea kwa hali ya juu mwaka 2014

Ujangili wa tembo umeendelea kwa hali ya juu mwaka 2014

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa mauaji haram ya tembo kwa mwaka 2014 yameendelea kwa kiwango cha juu ambacho kinaathiri uwepo kwa tembo katika siku za usoni. Taarifa ya Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti hiyo iliyotolewa na Mktaba wa kimataifa kuhusu biashara ya vyumbe vilivyo hatarini, CITES, imesema kiwango cha ujangili hakijaongezeka mwaka 2014 ikilinganishwa na 2013, lakini vile vile hakijapungua.

Halikadhalika, idadi ya mauaji ya tembo inazidi idadi ya tembo wanaozaliwa kila mwaka na kwa hiyo kuathiri uwepo wa tembo duniani.

Katibu Mkuu wa CITES John Scanlon amesema ujangili wa tembo kwa ajili ya pembe zake ni hatari kubwa sana kwa tembo waliopo barani Afrika, licha ya matumaini yatokanayo na jitithada zilizofanyika kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Maeneo ya wasiwasi zaidi kwenye bara hili ni pamoja na mbuga za wanayama za Selous, Mikumi na Ruaha zilizopo Tanzania, na Meru, Samburu na Laikipia nchini Kenya.