Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabunge yazingatie usawa wa jinsia: UN-Women/IPU

Mabunge yazingatie usawa wa jinsia: UN-Women/IPU

Haki za mwanamke si jambo la mjadala bali ni suala la kufikia ustawi wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge duniani, IPU, Martin Chungong katika kikao kuhusu mabunge na usawa wa kijinsia, kikao ambacho ni sehemu ya mkutano wa 59 wa kamisheni kuhusu hali ya wanawake unaoendelea mjini kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kikao hicho pamoja na kuangalia nafasi ya mabunge kinaangazia utekelezaji wa vipaumbele vya mkutano wa wanawake uliofanyika Beijing miongo miwili iliyopita na mustakhbali wa baadaye.

Bwana Chungong akasema mafanikio yamepatikana lakini mambo matatu yanapaswa kuzingatiwa ili kufikia usawa wa kijinsia..

(Sauti ya Chungong)

“Kuheshimu haki za wanawake, ushiriki sawa wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na mabunge thabiti na utawala wa kidemokrasia.”

Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women Phumzile Mlambo-Ngucka ambaye ni waandaji wenza wa kikao hicho amesifu mabunge ambayo yamepitisha sheria zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake lakini cha kufanya sasa ni kubadili mtazamo.

Lakini pia..

(Sauti ya Phumzile)

“Lazima tupate njia ya kushughulikia mvutano kati ya sheria nzuri zinazoshughulikia vizuri usawa wa kijinsia na sheria na tabia za kimila zinazokwamisha sheria hizo.”