Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Radio duniani, Kyela FM yaibuka kidedea

Siku ya Radio duniani, Kyela FM yaibuka kidedea

Kituo cha Radio cha Kyela FM mkoani Mbeya, kusini mwa Tanzania kimeshinda tuzo ya UNESCO ya uaandaaji wa vipindi vinavyogusa vijana na hivyo kualikwa nchini Ufaransa kwenye kilele cha maadhimisho hayo.

Al-Amin Yusuph mratibu wa masuala ya radio wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO nchini Tanzania ameieleza idhaa hii kuwa radio hiyo  ilizingatia mwongozo wa UNESCO uandaaji vipindi ambapo ..

(Sauti ya Al-Amin)

Naye Maisha Ambangile Meneja wa kituo hicho cha Kyela FM akatueleza msingi wa ushindi wao ni vipindi walivyoandaa kufuatia mafuriko ya mwezi Aprili mwaka 2014 huko Kyela.

(Sauti ya Maisha)

Mradi huo wa kushirikisha vijana kwenye kuandaa vipindi vya Radio unafadhiliwa na UNESCO kwa ushirikiano na shirika la SIDA-Sweden.