Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio itumiwe kupaza sauti za vijana:Ban

Radio itumiwe kupaza sauti za vijana:Ban

Katika maadhimisho ya siku ya Radio duniani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaka chombo hicho kitumiwe kupaza zaidi sauti za vijana ambao ni Bilioni Moja nukta Nane duniani kote. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Maadhimisho ya siku hii yanaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO ambapo Mkurugenzi wake mkuu Irina Bokova ametaka fursa zaidi za elimu na mafunzo kwa wanahabari vijana ili vipindi vyao viwe na mantiki.

Naye Katibu Mkuu Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa siku hii yenye maudhui ya umuhimu wa Radio kwa vijana ametambua nafasi ya chombo hicho  kinachobeba fikra na kuunganisha watu kila uchao, hivyo akasema..

 (Sauti ya Ban)

 “Jamii ya kimataifa inapoandaa malengo mapya ya maendeleo endelevu na makubaliano mapya ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, tunataka kusikia sauti za vijana wa kike na wa kiume, kwa nguvu, uthabiti na haraka.”