Skip to main content

Ban alaani mauaji ya mwanahabari Kenji Goto

Ban alaani mauaji ya mwanahabari Kenji Goto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari, Kenji Goto, raia wa Japan aliyeuawa na kundi la kigaidi linalotaka kuweka dola la Uislamu wenye msimamo mkali, ISIL au Daesh.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imesema, mauaji ya Goto yanaongeza kumulika ukatili ambao watu wengi wamelazimika kukumbana nao Iraq na Syria.

Ban amekariri wito wake wa kutaka mateka wote wanaoshikiliwa na Daesh na makundi mengine waachiliwe bila masharti, akituma rambi rambi zake kwa familia ya Goto, pamoja na serikali ya Japan na watu wake.