Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa ziarani Uganda

Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa ziarani Uganda

Sam Kutesa, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ameelezea mafanikio ya baraza hilo katika miezi iliyopita alipozungumza na waandishi wa habari mjini Kampala, wakati anapotembelea Uganda katika ziara yake ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika.

Miongoni mwa mafanikio aliyotaja ni vita dhidi ya Ebola, mchakato wa kuunda ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015, na makubaliano juu ya biashara ya silaha ndogo ndogo.

Halikadhalika, Rais wa Baraza Kuu amesema maswala yatakayopewa kipaumbele katika miezi ijayo ni ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015, maandalizi ya kongamano la mabadiliko ya hali ya hewa ya Paris, usawa wa kijinsia na mabadiliko ya mfumo wa baraza la usalama.

Aidha Sam Kutesa ameshiriki katika upandaji wa miti leo mjini Kampala, ili kusisitiza umuhimu wa kupambana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatimaye anatakiwa kuongoza mkutano kuhusu ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa jumanne hii, na kesho anakutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuelekea makao makuu ya Muungano wa Afrika, nchini Ethiopia.