Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brown ataka ulimwengu ulaani ukatili wa Boko Haram dhidi ya watoto

Brown ataka ulimwengu ulaani ukatili wa Boko Haram dhidi ya watoto

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Gordon Brown, amesema leo kuwa ulimwengu mzima unapaswa kuungana katika kulaani uovu mpya wa Boko Haram wa kutumia watoto wa kike kama walipuaji wa bomu wa kujitoa mhanga katika mashambulizi yao ya kikatili.

Bwana Brown ametaja mifano miwili, akianza na Ijumaa iliyopita pale bomu lililofungwa kwa msichana wa shule lilipolipuka katikati mwa mji wa Maiduguri, jimbo la Borno na kuwaua watu wapatao 20, na Jumapili, ambapo wasichana wawili walijiua sokoni katika mji wa Potiskum, jimbo ya Yobe, wakiwaua watu watatu na kuwajeruhi zaidi ya 40 wengine.

Brown amesema vitendo hivyo vimetokea wakati Boko Haram wakiwa wameuudhi ulimwengu kwa vitendo vyao vya kuwaua kiholela watu katika miji ya Baga na Doron Baga, akiwemo mama mmoja aliyekuwa akijifungua mimba. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Msemaji wa Katibu Mkuu, Stephane Dujarric amesema…

Bwana Brown amesema, wakati tukikaribia kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutekwa nyara kwa wasichana 200 wa shule ya Chibok, ni lazima tujitoe kuchukua hatua zaidi dhidi ya Boko Haram na kuhakikisha kuwa watoto wote wanalindwa vyema zaidi, kwa kuunga mkono mchakato wa Rais Goodluck Jonathan wa kuwa na shule salama.”