Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kufumbia Macho usafiri hatari wa wakimbizi baharaini: UNHCR

Hatuwezi kufumbia Macho usafiri hatari wa wakimbizi baharaini: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNCHR, limeelezea wasiwasi wake kuhusu mbinu mpya ya usafirishaji wa wakimbizi na wahamiaji barani Ulaya kwa kutumia meli kubwa ya Mizigo. Taarifa zaidi na Amina Hassan(TAARIFA YA AMINA)

UNHCR imesema, mataifa ya Ulaya hayawezi kufumbia macho mtindo huu kwani bila kuwepo kwa njia halali za wakimbizi na wahamiaji kuingia barani humo usafiri hatari wa meli hautapungua.

Ariane Rummery ni Msemaji wa UNHCR katika Ofisi ya Geneva

(Sauti ya Ariane Rummery)

“Wakati watu wanaangazia ulinzi wa mpakani, wasisahau masharti ya kibinadamu ya kuokoa maisha. Watu wasingeshiriki safari ya boti na kulipa maelfu ya dola na kwa hivyo kuwa mikonono mwa wasafirishaji haramu wasio na huruma ikiwa hawana hawana sababu nzuri”

Aidha, UNHCR imeshukuru Serikali ya Italia kwa  hatua yao ya uokozi wa hivi karibuni licha ya kusitishwa kwa Operesheni ya Mare Nostrum.