Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA Tanzania yaendesha kambi za mafunzo ya ukeketaji, ndoa za utotoni na tohara asilia.

Kampeni ya UNFPA Tanzania@UNFPA/TZ

UNFPA Tanzania yaendesha kambi za mafunzo ya ukeketaji, ndoa za utotoni na tohara asilia.

Katika kusongesha juhudi za kampeni dhidi ya  ndoa za utotoni, ukeketaji na tohara za njia za asili , Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania limenzisha kambi maalum mkoani Mara zinazotoa mafunzo  mbadala.Kwa mujibu wa afisa mawasiliano wa UNFPA nchini Tanzania Sawiche Wamunza kambi hizo zimeelekezwa mkoani humo ambako vitendo hivyoo hufanyika kwa wingi.

(SAUTI WAMUNZA)

Hata hivyo Bi Wamunza amesema licha ya juhudi hizo, kuna mengi ya kufanya ili kutokomeza kabisa ndoa za utotoni, ukeketaji na  tohara za asilia.

(SAUTI WAMUNZA)