Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yakaribisha usafiri wa msaada kupitia mto Nile

Msaada wa chakula.(Picha ya WFP/Sudan Kusini)

WFP yakaribisha usafiri wa msaada kupitia mto Nile

Msaada huo wa tani 450 utasaidia katika kulisha watu takriban 28,000 kwa mwezi moja kama sehemu ya mradi uliozinduliwa mwezi Novemba wa kufikisha chakula nchini Sudan Kusini kupitia Sudan. Kaimu msimamizi wa WFP nchini Sudan kusini Stephen Kearney amesema kwamba hii ni mara ya kwanza ambapo Shirika hilo limeweza kuwasilisha chakula kupitia mpaka wa nchi hizo mbili  na kusema kwamba hatua hii itabadilisha juhudi zao za kutoa msaada kwa walio na mahitaji ya dharura. Challiss McDonough ni msemaji wa WFP mjini Nairobi.

"Tumekuwa tukitegemea usafiri wa anga kwa mwaka mmoja kwa sababu ya kufungwa kwa barabara kwa sababu ya mvua na ukosefu wa usalama kwa hivyo kama tunaweza kutumia usafiri wa barabara na mto kufikia maeneo ya kaskazini mwa Sudan Kusini hiyo itatuwzesha kupunguza matumizi ya usafiri  kwa asilimia 6-7  ya usafiri wa anga kusafrisha chakula.”

Usafiri wa misaada kupitia mto Nile kati ya Sudan na Sudan Kusini ulisimamishwa baada ya kufungwa kwa mpaka kufuatia Sudan Kusini kupata uhuru mwaka 2011. Usafiri wa mto umewezeshwa na serikali za nchi hizo mbili na uelewa wa pande zote kuhusu umuhimu wa kuwezesha usafiri wa msaada wa kibinadamu kwa wananchi walioathiriwa na mzozo nchini Sudan Kusini.