Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kikanda ni muhimu katika kukabiliana na majanga:ESCAP

Picha@UNESCO

Ushirikiano wa kikanda ni muhimu katika kukabiliana na majanga:ESCAP

Wakati tukielekea maadhimisho ya miaka kumi tangu janga la Tsunami kutokea kusini na kusini Mashariki mwa Asia mengi yamefanywa kuziba pengo katika kuzuia majanga, kupunguza hatari na kuimarisha vifaa vya kutahadharisha dhidi ya janga ambalo lilisababisha watu takriban 230,00 kupoteza maisha na zaidi ya milioni tano kuathiriwa  Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRACE)

Umoja  wa Mataifa kupitia  Tume ya uchumi na kijamii kwenye ukanda wa Asia Pasifiki, ESCAP iko mstari wa mbele katika kuwezesha juhudi za ukanda huo, kuimarisha teknolojia mpya na kuendeleza miradi ya kutoa tahadhari ya mapema kupitia mfuko wake wa Tsunami, majanga na mabadiliko ya hali ya hewa. Bi Shamika Sirimanne ni mkurugenzi wa mawasiliano kitengo cha kupunguza majanga, ESCAP

Kama ukanda tumepiga hatua tangu janga la Tsunami, tuko tayari kuliko mwaka 2004, tuna vifaa vinavyostahili ambavyo vinahitji kurekebishwa na kuimarishwa, kuna kazi nyingi ya kufanya hususan kuhakikisha kwamba walio hatarini zaidi na katika maeneo ya vijijini wanapata taarifa kuhusu tahadhari kwa wakati sahihi, ushirikiano wa kikanda ni muhimu.”

Janga la Tsunami lilitokea Disemba 26 mwaka 2004 na linatajwa kama moja ya majanga mabaya zaidi kuwahi kutokea.