Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya Udongo, tulinde rutuba yake: FAO

Udongo wenye rutuba huwezesha kupata mazao bora. (Picha@Unifeed)

Siku ya kimataifa ya Udongo, tulinde rutuba yake: FAO

Udongo wenye rutuba ni muhimu kwa uzalishaji wa mazao bora duniani, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva katika ujumbe wake wa siku ya udongo duniani Disemba Tano.

Amesema udongo wa aina hiyo siyo tu ni msingi wa chakula, nishati na hata dawa bora  bali pia ni muhimu kwa baionuai kwani inaweza mzungumzo wa hewa ya ukaa, unachuja maji na kuwezesha ustahimilivu wakati wa mafuriko na ukame.

Bwana da Silva amesema kutokana na umuhimu huo ni vyema kuepuka uharibifu wa mazingira unaotishia udongo wenye rutuba kwa kuwa uzalishaji wa chakula kwa watu zaidi ya Milioni 805 wenye njaa duniani kote utakuwa mashakani.

Ametaka hatua zichukuliwe kulinda rutuba ya kwenye udongo akisema kuwa siku hii inakwenda sambamba na uzinduzi wa mwaka wa kimataifa wa udongo 2015, uzinduzi unaofanyika Roma, Italia.