Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Sudan Kusini waongezeka Uganda

Mvulana huyu ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini na ni miongoni mwa watu waliokimbilia nchi jirani, Uganda(Picha © UNHCR/F.Noy)

Wakimbizi wa Sudan Kusini waongezeka Uganda

Mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini umesababisha wimbi jipya la raia wake wanaokimbilia nchi jirani hususani Uganda. Katika wiki iliyopita, takribani wakimbizi 1,600 waliingia nchini kumo kupitia mipaka mbali mbali kama anavyoripoti John kibego wa redio washirika Spice FM ilioko Hoima nchini humo. Taarifa ya John Kibego.

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) humo nchinim ameniambia, wakimbizi 1,530 walipokewa kati ya tarehe nne na tarehe kumi za mwezi huu wa Disemba.

Lucy Beck amefafanua kuwa, wengi wanaingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu na kwa sasa wanahifadhiwa katika kambi za Kiryandongo, Arua na Adjuman.

Wengi wametoroka Jimbo la Eastern Equatoria kufuatia hofu ya kuzuka kwa makabiliano kati ya jeshi la serikali ya Sudan Kusini na wapiganaji wanaomtii Kamanda Martin Kenyi anayoripotiwa kukwepa jeshi hilo.

Lakini, alipotembelea maeneo ya Pagari, Gavana wa Jimbo hilo Louis Labong alifutilia mbalai tarifa kwamba Kamanda Kenyi ameanza kuwakusanya waasi wa zamani wa Equatoria Defense Forces (EDF).

Aliwaomba wananchi kutulia majumbani na kusema, Kamanda huyo alikwenda Uganda kwa ajiili ya matibabu na wala haana mpango wa kuaasi.