Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la pili la wakimbizi wa Somalia larejea nyumbani kutoka Kenya

Wakimbizi wa Somalia wanaorejea nymbani kwao kwa hiari.(Picha ya UNHCR/Kenya/facebook)

Kundi la pili la wakimbizi wa Somalia larejea nyumbani kutoka Kenya

Kasi ya kuwarejesha kwa hiari wakimbizi wa Somalia wanaoishi nchini Kenya inazidi kupanda, na kufikia sasa, kwa mujibu wa Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi, UNHCR wakimbizi 179 wamerejea nchini Somalia.

Kundi la pili la wakimbizi 88 limerejea tarehe 11 mwezi huu baada ya lile la kwanza likiwa na wakimbizi 91 kurejea nyumbani tarehe Nane.

Katika mahojiano na idhaa hii, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Kenya, Emmanuel Nyabera amesema kuna wakimbizi wengi ambao wameonyesha nia ya kurudi baada ya kuwasiliana na wenzao waliokwenda.

(SAUTI NYABERA)

Japo Shirika al Umoja wa Mataifa linawasaidia wakimbizi wanaotaka kurudi kwa hiari, Bw Nyabera anasema kuna change moto zinazowafanya baadhi ya wakimbizi wasite kurudi.

(SAUTI NYABERA)