Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo nchini Ukraine waathiri mustakhbali wa raia:Ripoti

Mfanyakazi wa UNHCR azungumza na mwanamume aliyefurushwa kutoka makazi yake katika eneo la Donetsk ambako kumeathiriwa na mzozo.Picha© UNHCR/I.Zimova

Mzozo nchini Ukraine waathiri mustakhbali wa raia:Ripoti

Wakati msimu wa majira ya baridi kali ukiendelea kushika kasi huko Ukraine, raia wanaoishi kwenye maeneo yenye mapigano kati ya vikosi vya serikali na vile vinavyotaka kujitenga wanazidi kukumbwa na mazingira magumu.

Hiyo ni kwa mujbu wa ripoti iliyotolewa leo na Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyoangazia matukio ya mwezi Novemba wakati huu ambapo makubaliano ya kusitisha mapigano yamekuwa hatarini.

Gianni Magazzeni, mwakilishi kutoka ofisi ya haki za binadamu anasema miezi Tisa tangu kuanza mapigano hali ya haki za binadamu inazidi kuzorota hususan mashariki mwa nchi hiyo.

 (Sauti ya Magazzeni)

"Kuendelea kwa vitendo  vya mauaji , kutekwa nyara, mateso, ukatili wa kingono , ubakaji, utumikishwaji , kutozwa fidia na ukiukwaji wa sheria huko maeneo ya Mashariki mwa Ukraine yanayoshikiliwa na vikundi vilivyojihami . Hakuna utaratibu au uhakika wa ulinzi wa watu walioko eneo hilo na ambao walioko mikononi mwa watu hao waliojihami.”

Ripoti ya leo ni ya Nane wakati huu ambapo mzozo wa Ukraine umesababisha vifo vya watu 4,700 majeruhi 10,300 na takribani Milioni Moja wamesalia wakimbizi.