Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO alaani mauaji Kivu kaskazini

Martin Kobler (katikati) mkuu wa MONUSCO akiwa na baadhi ya maafisa na askari kutoka jeshi la serikali FARDC na lile la kuingilia kati mashambulizi, (FIB) walipofanya ziara karibu na eneo la Tongo, Mashariki mwa DRC. (Picha: UN /Sylvain Liechti)

Mkuu wa MONUSCO alaani mauaji Kivu kaskazini

Mkuu wa vikosi vya operesheni ya amani ya Umoja wa Mataifa katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. MONUSCO,  Martin Kobler amelaani vikali tukio la mashambulizi yaliyofanywa jana usiku na kusababisha mamia ya raia kuuawa kwenye maeneo ya  Ahili na Manzanzanba jimbo la Kivu Kaskazini. Taarifa zaidi na George Njogopa(TAARIFA YA GEORGE)

Katika taarifa yake kuhusiana na mauwaji hayo mkuu huyo wa MONUSCO amesema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama ambacho kinaweza kufungua milango ya kukaribisha vitendo vya kigaidi katika eneo hilo.

Huku akielezea masikitiko yake kutoka na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, Kobler amesema kuwa katika jinsi yoyote mauaji hayo yanapaswa kusitishwa mara moja na kuzikata pande zenye hasimiana kurejea mezani kwa mazungumzo.

Alisema kuwa kunahitajika ushirikiano wa dhati toka vikoso vya serikali na vile vya kimaifa ili kukabiliana na hujuma zinazoendele kuliandama eneo hilo .

Kundi la watu wasiojulikana jana usiku walivamia maeneo mawili na kusababisha mauajia kwa raia wasiokuwa na hatia. Kumekuwa na hali ya sintofahamu katika jimbo la Kivu ya Kaskazini kutokana na kujitokeza kwa mashambulizi ya mara kwa mara na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.