Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukomesha Ukatili Dhidi ya Wanawake ni hatua muhimu ya kutokomeza njaa:WFP

Wakulima.(Picha ya WFP/Marco Frattini)

Kukomesha Ukatili Dhidi ya Wanawake ni hatua muhimu ya kutokomeza njaa:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema kutokomeza njaa ni mojawapo ya njia za kumaliza ukatili huo. WFP imetolea mfano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo wanawake wanaokwenda kusaka chakula au kuchanja kuni wako hatarini kubakwa ikisema kila siku kwa wastani wanawake na wasichana 36 hubakwa.

Wakati huo huo Mkuu wa kutokomeza ukatili kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women Riet Groenen amesema ukatili dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

 (Sauti ya Riet)

 "Ukatili unatokea kila nchi duniani. Haijalishi  kama wewe ni tajiri au maskini, una elimu au la.  Ni bahati mbaya sana jambo hili hukumba wasichana wengi o. Aina inayojulikana zaidi ni ukatili unaofanywa na mpenzi ambao hujulikana kama ukatili wa majumbani.”