Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makazi ya wapalestina yaachwe kulengwa: Mtaalamu

UN Photo/Violaine Martin
Makarim Wibisono.

Makazi ya wapalestina yaachwe kulengwa: Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo kaliwa ya Palestina na haki ya makazi Makarim Wibisono ameitaka Israel iache kubomoa makazi ya wapalestina kwa madai kuwa ni hatua dhidi ya ghasia zinazofanywa na wapalestina dhidi ya Israeli.

Ametolea mfano tukio la tarehe 19 mwezi huu ambapo majeshi ya Israel katika kubomoa makazi ya mpalestina huko Yerusalem Mashariki anayedaiwa kuhusika na shambulio lililosababisha vifo vya raia wawili wa Israeli, yaliharibu pia makazi ya kaya zingine kwenye jengo hilo la makazi.

Wibisono amesema vitendo vya ghasia vinahitaji hatua kutoka serikali ya Israeli na wahusika wafikishwe mbele ya sheria lakini serikali haiwezi kukiuka kanuni zinazotambuliwa na sheria ya kimataifa.