Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wachunguzi wa Haki za Binadamu wa UM wazuiwa kukamilisha uchunguzi wao Gambia.

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji kinyume na sheria, Christof Heyns.(Picha:Jean-Marc Ferré)

Wachunguzi wa Haki za Binadamu wa UM wazuiwa kukamilisha uchunguzi wao Gambia.

Wataalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Christof Heyns na Juan Méndez, wamezuiwa kukamilisha uchunguzi wao kuhusu mateso na mauaji wakati wa ziara yao ya kwanza nchini Gambia, kama sehemu ya utaratibu  wa Baraza la Haki za Binadamu.

Wataalamu hao wawili waliwasilisha ujumbe rasmi kwa nchi hiyo wa kuchunguza kiwango cha sasa cha ulinzi wa haki ya kuishi katika sheria na vitendo, na kutathmini hali na kutambua changamoto kuhusu mateso na ukatili mwingine, unyama na udhalilishaji nchini Gambia, miongoni mwa mambo mengine.

Katika hatua ya kutia moyo, Serikali ya Gambia iliwaalika wataalamu hao wawili wa Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu kufanya ziara ya pamoja kuanzia Novemba 03-07 2014. Lakini kwa bahati mbaya, na licha ya makubaliano ya mwongozo wa utendaji kazi katika maandishi, wapelelezi hao walipowasili  nchini serikali iliwazuia kutembelea gereza fulani kama walivyokubaliana awali.