Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EAC wajadili sera endelevu katika mazingira na usalama wa chakula.

Chakula.@FAO

EAC wajadili sera endelevu katika mazingira na usalama wa chakula.

Wawakilishi wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana mjini Bujumbura Burundi kujadili uhusiano uliopo kati ya mabadiliko ya tabia nchi,mazingira, biashara na usalama wa chakula lengo likiwa ni kuhakikisha sera za kila eneo hazisigani na hivyo kuwa endelevu.

Katika mahojiano na idhaa hii mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa  Mataifa mjini Geneva balozi Modest Mero  licha ya kufafanua kinachojadiliwa anasema  kubadili tabia ndiyo changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi

(SAUTI MERO)