Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yahaha kunusru mji mkongwe Zanzibar usifutwe kwenye orodha ya urithi wa dunia

Mki mkongwe nchini Zanzibar© UNESCO

UNESCO yahaha kunusru mji mkongwe Zanzibar usifutwe kwenye orodha ya urithi wa dunia

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO linahaha kunusuru na kurejesha hadhi ya mji mkongwe wa Zanzibar ambao umeingia katika orodha hatarishi ya kutoweka katika urithi wa dunia.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii afisa wa UNESCO Tanzania Moshi Kiminzi amesema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali ya Zanzibar na mamlaka ya mji mkongwe wanahakikisha hatua muhimu zinachukuliwa kunusuru mji huo ambao amesema kutoweka kwake kutafuta historia ya eneo hilo muhimu Afrika Mashariki

(SAUTI KIMINZI)

Pia Bwana Kiminzi amefafanua kile kinachofanywa na UNESCO kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutunza mji huo ili usiondoke katika orodha ya urithi wa dunia.

(SAUTI KIMINZI)

Mahojiano kamili kuhusu taarifa hii yatapatikaan kwenye ukurasa wetu.