FAO kuzisaidia kaya zilizoathirika na ebola Afrika magharibi

Onyo kuhusu atahri za ebola mjini Freetown.Agosti 2014.Picha ya FAO

FAO kuzisaidia kaya zilizoathirika na ebola Afrika magharibi

Shirika la mpango wa chakula duniani limepanga kuzindua mpango maalumu kwa ajili ya kuzikwamua zaidi ya familia 90,000 zilizoathirika na homa ya ebola katika nchi  za Liberia, Guinea na Sierra Leone.

FAO katika mpango huo imepanga kusambaza msaada wa chakula kwa kaya hizo ambazo zimeshindwa kuendelea na shughuli za kilimo kutokana na kukubwa na tatizo la homa hatari ya ebola.Taarifa kamili na  George Njogopa

(Taarifa ya George)

Mpango wa kikanda utaongeza kasi ya miradi mingine inayotekelezwa na shirika hilo katika eneo la Afrika magharibi, eneo ambalo limekuwa likiandamwa na tatizo la ebola tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

FAO kwa kushirikiana na serikali katika eneo hilo na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa imepanga kuendesha mkakati maalumu utakaohakikisha kwamba usambaaji wa magonjwa pamoja na matatizo mengine inakuwa historia.

Kwa hivi sasa shirika hilo limesema kuwa linahitaji kiasi cha Dola za Marekani milioni 30 kwa ajili ya kufanikisha miradi yake ambayo imepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Katika kufanikisha makakati huu FAO imeanzisha sera ya mifugo itakayosaidia kuwakwamua raia katika kutumia vyakula vya porinikamaanayoeleza afisa mifugo Juan Labroth

(SAUTI JUAN)

Sisi FAO tunatuambua kuwa kutumia vyakula vya misituni ni hatari na hivyo tunapendekeza sera bora ya mifugo mathalani kuku ambayo inaweza kusaidia kuepuka kutumia vyakula vya porini ili hili lisijitokeze tena