Wengi wanaathiriwa na mapigano Ukraine

8 Oktoba 2014

Pamoja na mpango wa usitishwaji wa mapigano uliofikiwa mwezi iliopita hukoUkrainelakini mapigano makali yameendelea kujitokeza katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha mamia ya raia kupoteza maisha.

Hayo ni kwa mujibu ripoti mpya iliyozinduliwa na Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein aliyeangazia hali ya mambo nchini humo.

(Taarifa ya Grace)

Licha ya kwamba ripoti zinasema kwamba katika kipindi cha kuanzia Septemba 5 mwaka huu kulikoasisiwa mchakato huo wa amani, kuonyesha kutokuwepo kwa mapigano ya hali ya juu lakini katika baadhi ya maeneo hali ni tofauti kidogo.

Mapigano makali yamekuwa yakiukumba uwanja wa ndege waDonetskna maeneo mengine ya jirani na kusababisha  hofu kubwa kwa wakazi wa eneohilo.

Kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu amesema kuwa zaidi ya watu 3,660 wamepoteza maisha tangu kuzuka kwa machafuko hayo mwezi April mwaka huu.

Kamishna huyo Hussein ameongeza pia mapigano hayo  yamesababisha zaidi ya watu 8,756 kujeruhiwa huku wengine wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter