Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya walimu nchini Kenya bado si asimilia mia kwa mia

UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Mwalimu wa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk, Darfur Kaskazini.

Hali ya walimu nchini Kenya bado si asimilia mia kwa mia

Wakati siku ya walimu duniani ikiadhimishwa Oktoba 5 Shirika la kazi duniani ILO limesema kiwango cha elimu kinategemea uwezo wa walimu likisema kuwa walimu bora ni muhimu kwa kiwango bora cha elimu ya u mma.

ILO hata hivyo inasema kiwango cha elimu kinadunishwa na upungufu wa walimu bora ambapo walimu zaidi ya Milioni 1.4 wanahitajika katika madarasa kote ulimwenguni ili kutoa elimu ya msingi kwa wote.

Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii katibu mkuu wa chama cha walimu nchini Kenya KNUT, William Sossion amekiri kuwepo kwa changamoto hizo.

(Sauti ya Sossion)

Bwana Sossion amesema kiungo muhimu katika kuboresha elimu ni kuzingatia teknolojia za kisasa.

(Sauti ya Sossion)

Halikadhalika amesema kwamba KNUT itatumia siku hii ya walimu katika kuhamashisha serikali ya Kenya kuzingatia sera amabazo zitaweza kuboresha mustakhabali wa walimu nchini humo.