Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UN wampongeza Obama

Rais Barack Obama wa Marekani akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Mark Garten)

Wataalamu wa UN wampongeza Obama

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekaribisha tangazo lililotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani aliyesema kuwa serikali yake itaanzisha mkakati mpya wa uendeshaji wa biashara katika mazingira ya uwazi na uwajibikaji mkakati ambao unakwenda sambamba na misingi ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia mpango huo wa Rais Obama, mmoja ya watalaamu hao wa Umoja wa Mataifa Michael Addo alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kutoa fursa kwa watu na hata makundi ya watu ambao wanakandamizwa sauti zao kusikilizwa.

Katika tangazo lake, Rais Obama alisema kuwa Marekani iko mbioni kuanzisha mkakati wa kitaifa ambao utahakikisha kwamba mifumo ya ufanyaji biashara inakuwa ya uwazi tena wahusika wake watawajibika kwa lolote.