Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa Colombia kutunukiwa tuzo ya UNHCR

waratibu wa Butteflies ambao wanafanya kazi kwa kujitolea kuwasaidia wanawake waliofurushwa makwao kufuatia ukatili.Picha ya UNHCR/L.Zanetti

Wanawake wa Colombia kutunukiwa tuzo ya UNHCR

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi António Guterres atakabidhi tuzo maalumu kwa wanawake  wa Colombia kama sehemu ya kutambua mchango wao wa kuwapiga jeki watu waliokumbwa na majanga ikiwamo wale waliokosa makazi.

Wanawake hao Gloria Amparo, Maritza Asprilla Cruz na Mery Medina wamekuwa wakiitumia taasisi yao kuwasaidia watu mbalimbali wanakumbwa na matatizo ikiwamo wale wanakumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.

Wote kwa pamoja wanaripotiwa kuwasaidia zaidi ya wanawake 1000 na watoto wao ambao wamekumbwa na matukio mbalimbali.  Colombia inatajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu waliokosa makazi kutokana na machafuko ya mara kwa mara.

Tuzo hiyo itakayotolewa leo Jumatatu usiku ni miongoni mwa tuzo za hali ya juu zinazotolewa na UNHRC kwa watu wanawasaidia watu wanaokumbwa na hali ngumi.