Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi mabaya ya dawa ya chanjo yalisababisha vifo vya watoto Syria- WHO

Nembo ya WHO.(Picha ya UM/maktaba)

Matumizi mabaya ya dawa ya chanjo yalisababisha vifo vya watoto Syria- WHO

Tathimini ya Shirika la Afya Duniani, WHO, imebaini kuwa vifo vya watoto 15 vijijini Idleb, kaskazini mwa Syria vilitokana na matumizi mabaya ya dawa ya iitwayo Atracurium, ambayo hutumiwa kuzimua dawa ya chanjo ya surua.

WHO imesema kuwa hakuna ushahidi kuwa matumizi mazuri ya chanjo ya Surua/Rubella yenyewe au kizimuzi chake, Atracurium yalisababisha vifo hivyo. Kwa kawaida, dawa ya chanjo ya surua huzimuliwa kabla ya kutumiwa.

WHO imesema kuwa vidonge vya Atracurium vilichanganywa vibaya na dawa za chanjo zilizoandaliwa katika kituo kimoja cha kuandaa dawa hizo kwa kuzisambaza, katika kata ya Idleb.

Chanjo ni njia moja ya msingi zaidi ya kuzuia ugonjwa wa kuambukiza, na tishio la surua nchini Syria.