Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mazungumzo na Rais Cristina Fernández wa Argentina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na Rais Cristina Fernández wa Argentina.Picha ya UM/Eskinder Debebe

Ban afanya mazungumzo na Rais Cristina Fernández wa Argentina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Cristina Fernández wa Argentina leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Ban na Rais Fernández wamejadili kuhusu deni la Argentina na jinsi linavyoathiri juhudi za taifa hilo kubadilisha deni la kigeni.

Katibu Mkuu amesema kuwa hili ni suala muhimu ambalo nchi wanachama zinapaswa kujadili zaidi.

Bwana Ban pia ameelezea shukran zake kuhusu michango muhimu ya Argentina kwa Umoja wa Mataifa, ikiwemo ya walinzi wa amani na kama mwanachama wa Baraza la Usalama. Wamebadilishana mawazo pia kuhusu masuala ya kimataifa, yakiwemo wanawake, vijana na elimu.