Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatuma jopo kuchunguza vifo vya watoto Syria, kampeni ya chanjo yasitishwa

Watoto wa Syria walio kwenye kambi za wakimbizi. (Picha:UM)

WHO yatuma jopo kuchunguza vifo vya watoto Syria, kampeni ya chanjo yasitishwa

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la afya, WHO na lile la kuhudumia watoto, UNICEF yameelezea kushtushwa na masikitiko juu ya vifo vya watoto 15 hukoIdilib,Syriavilivyotokea kwenye maeneo ambamo kampeni ya chanjo dhidi ya Surua ilikuwa inaendelea. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Taarifa ya pamoja ya mashirika hayo imesema jukumu ya jopohiloni kutoa usaidizi kwa wataalamu wanaochunguza kisa hicho na hatimaye watoe ripoti haraka iwezekanavyo huku WHO ikitoa ushauri na mwongozo kufuatia taarifa hizo zisizo njema baada ya chanjo.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema uamuzi wa kusitisha kampeni ya chanjo kwenye majimbo ya Idlib na Deir Ezzour bado unabakia ni hatua sahihi zaidi kwa kuwa bado chanzo cha vifo vya watoto hao hakijajulikana.

Hata hivyo amesema..

(sauti ya Christian)

“Kwa kweli changamoto kubwa itakuwa ni kurejesha imani kwenye jamii, kwa sababu kama mnavyojua kampeni ya chanjo ya surua ni muhimu sana, Surua ni ugonjwa hatari ambao unaua watoto wengi wenye umri tofauti. Kwa hiyo kampeni ya surua katika nchi iliyokumbwa na mgogoro wa kivita ni muhimu sana.”

WHO imesema itakuwa ni vyema kampen ikaendelea haraka iwezekanavyo kwani Surua ni ugonjwa tishio kwa watoto wanaoishi kwenye maeneo yasiyosafihususan hukoSyriaambako watoto wamekimbia makaziyaokutokana na mizozo na wanaishi kwenye kambi.