Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wakusanyika New York kupaza sauti juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Mary Robinson.Picha@UM

Wanawake wakusanyika New York kupaza sauti juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Wakati viongozi wa dunia wakikusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwa ajili ya mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi, zaidi ya wanawake 130 watakusanyika kutoka nchi 54 wakiwakilisha makundi mbalimbali wakiwemo wale wa mashinani, wanawake asilia, wasichana na wasomi kupaza sauti zao kuhusu ushiriki na ubia wao unaochochea usawa katika mambo ya tabianchi.

Makundi hayo ya wananawake yatakuwa na mkutano na marais wa zamani wa nchi mbalimbali hususani wanawake mathalani yule wa Malawi Joyce Banda, Mary Robinson wa Norway ma Helen Clark wa New Zealand.

Mkutano huo utaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake UN women ambapo mkurugenzi wake Phumzile Mlambo-Ngcuka na mwasisi wa Mary Robisnon Foundation Bi Mary Robisnon ambapo masuala ya wajibu na mahitaji ya wanawake katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi yatamulikwa.

Akizungumzia tukio hilo rais mstaafu wa Ireland Mary Robinson amesema katika kutunga sera za makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ni lazima kujumuisha watu ambao ndiyo wanaoathiriwa zaidi na janga hilo pamoja na kuheshimu haki ya ushiriki katika mchakto wa kufanya maamuzi.