Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la kusikiliza kesi dhidi ya Gbagbo latangazwa:ICC

Jopo la kusikiliza kesi dhidi ya Gbagbo latangazwa:ICC

Rais wa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC ameunda upya jopo la majaji litakaloendesha kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Ivory Coast, Lauren Gbagbo.

Taarifa ya ICC imetaja jopo hilo majaji Cuno Tarfusser kutoka Italia, Olga Herrera-Carbuccia kutoka Jamhuri ya Dominika na Geoffrey Henderson kutoka Trinidad na Tobago.

Tarehe 12 mwezi Juni mwaka huu jopo la majaji lilithibitisha kwa kauli ya wengi mashtaka manne dhidi ya uhalifu wa kibinadamu yanayomkabili Gbagbo na hivyo kutaka kesi yake ianze kusikilizwa.

Makosa hayo ni mauaji, ubakaji, utesaji na jaribio la kuua.

Tarehe 11 mwezi huu jopo tangulizi la majaji lilitupilia mbali ombi la upande wa utetezi la kuomba kibali ili likate rufaa kupinga uthibitishwaji wa makosa hayo,

Gbagbo alisamilishwa kwenye mahakama hiyo na uongozi wa serikali ya Ivory Coast tarehe 29 Novemba mwaka 2011 kufuatia kibali cha kukamatwa kwake kilichotolewa na mahakama ya ICC tarehe 23 Novemba 201